• HABARI MPYA

  Thursday, May 18, 2017

  CANNAVARO: TUNAKWENDA MWANZA KULIPA KISASI KWA MBAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanaelekea Mwanza kwenda kulipa kisasi kwa Mbao FC katika mchezo wa mwisho utakaopigwa CCM Kirumba.
  Yanga wanashuka dimbani Jumamosi ya mwishoni mwa wiki hii, wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 na Mbao katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sport – Online jana, Cannavaro alisema wanaenda kucheza na Mbao wakijihami na kuhakikisha wanawashusha daraja.
  Alisema wanashuhuru kupata ushindi katika mchezo na Toto kwa kupata ushindi wa bao moja na sasa kuelekeza nguvu katika mchezo wao huo na Mbao.
  Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanakwenda Mwanza kulipa kisasi kwa Mbao FC  

  Alisema kitendo walichowafanyiwa wanahitaji kulipa kisasi katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
  "Tunawafahamu Mbao walitufunga katika mchezo wa nusu FA, hivyo tunafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita na kutojitudia tena," alisema Cannavaro.
  Nahodha huyo alisema pia amependekeza majina ya baadhi ya wachezaji ambao watasaidia timu yao kufanya vizuri kwa msimu ujao wa ligi hiyo na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CANNAVARO: TUNAKWENDA MWANZA KULIPA KISASI KWA MBAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top