• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2017

  CAMEROON YATUPWA NJE FAINALI ZA U-17 AFRIKA

  TIMU ya Cameroon imetupwa nje ya Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17, licha ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gabon kwenye mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Port Gentil.
  Ushindi huo haujatosha kuwafanya wabaki kwenye mashindano na kukata tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia za FIFA U-17 Oktoba mwaka huu nchini India, baada ya Guinea kulazimisha sare ya bila kufungana na Ghana katika mchezo mwingine wa Kundi A leo mjini Libreville.
  Wachezaji wa Cameroon na Gabon wakiwania mpira wa juu leo

  Cameroon inaungana na Gabon kuaga mashindano baada ya hatua ya makundi, kutokana na kumaliza nafasi ya tatu mbele ya wenyeji, walioshika mkia, huku Guinea ikimaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tano na kuungana na Ghana iliyoongoza Kundi kwa pointi zake saba kwenda Nusu Fainali.
  Sasa Ghana na Guinea zitasubiri mechi za mwisho za Kundi B kesho kujua wapinzani wao wa Nusu Fainali.
  Tanzania itamenyana na Niger mjini Port Gentil na Mali itamalizana na Angola mjini Libreville. Mali na Tanzania zinafungana kwa pointi nne kila mmoja, mabao mawili ya kufunga na moja la kufungwa baada ya kushinda, wakati Angola na Niger zina pointi moja kila mmoja. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YATUPWA NJE FAINALI ZA U-17 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top