• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2017

  CAMEROON NI KUFA NA KUPONA LEO DHIDI YA GABON

  Na Mahmoud Zubeiry, PORT GENTIL
  MECHI za Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinahitimishwa leo na Cameroon itajaribu kuungana na Ghana kufuzu Nusu Fainali.
  Cameroon watamenyana na vibonde wenzao, wenyeji Gabon kuanzia Saa 12:30 jioni katika mchezo utakaochezeshwa na refa Mustapha Ghorbal wa Algeria, atakayesaidiwa na washika vibendera, Lahcen Azgaou wa Morocco na Temesgin Samuel Atango wa Ethiopia Uwanja wa Port Gentil.
  Na baada ya kufungwa 4-0 na Ghana na kutoa sare ya 1-1 na Guinea, Cameroon watahitaji kuifunga Gabon leo na huku wakiiombea dua mbaya Guinea ifungwe na Black Starlets ili wao waende Nusu Fainali.
  Ghana na Guinea watamenyana kuanzia Saa 12:30 pia Uwanja wa l’Amittiee mjini Libreville, katika mchezo utakaochezeshwa na refa Hamada el Moussa Nampiandraza wa Madagascar, atakayesaidiwa na washika vibendera Aymen Ismail wa Tunisia na Souru Phatsoane wa Lesotho.
  Pamoja na kwamba imekwishajihakikishia Nusu Fainali, lakini Ghana bado itahitaji ushindi ili kujiwekea mazingira ya kukutana na timu nafuu katika hatua hiyo.
  Mechi za mwisho za Kundi B zitachezwa kesho, Tanzania na Niger Uwanja wa Port Gentil na Mali na Angola Uwanja wa l’Amittiee.
  Mali na Tanzania zitaingia kwenye mechi za kesho zikihitaji hata sare ili kujihakikishia Nusu Fainali baada y azote kushinda mechi moja na sare moja katika mbili za awali. Sare ya 0-0 ni katika mechi ya baina yao, kabla ya Tanzania kushinda 2-1 dhidi ya Angola na Mali kuifunga 2-1 Niger katika mechi zilizofuta.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON NI KUFA NA KUPONA LEO DHIDI YA GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top