• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2017

  ULIMWENGU AWAKUMBUSHA MKUDE, MSUVA NA HAJIB DILI ZA SAUZI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amewashauri wachezaji wenzake wa timu ya taifa, Taifa Stars kiungo Jonas Gerlad Mkude, winga Simon Happygod Msuva na mshambuliaji Ibrahim Hajib Migomba kupigania nafasi za kwenda kucheza Afrika Kusini wakakuze uwezo wao.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu jana kutoka Sweden, Ulimwengu alisema kwamba watatu hao wote wana uwezo wa kucheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini, hivyo wanapaswa kutilia mkazo suaoa hilo.
  Thomas Ulimwengu amewashauri Mkude, Msuva na Hajib kupigania nafasi za kwenda kucheza Afrika Kusini wakakuze uwezo wao.

  Na kauli hiyo ya Ulimwengu inafuatia wachezaji wote hao kwenda Afrika Kusini kwa majaribio mwa jana kwa wakati na timu tofauti, Mkude na Msuva Bidvest Wits na Hajib Lamontville Golden Arrows FC za Ligi Kuu ya ABSA nchini humo na wote waliripotiwa kufuzu.
  “Mimi nadhani tujitahidi kuwahamasisha wachezaji wetu wa timu ya taifa waende hata Afrika Kusini kucheza, itasaidia sana kuliko kubaki wanacheza hapo hapo nyumbani,”alisema mshambuliaji huyo wa AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden.
  Ulimwengu alisema anafahamu Mkude, Msuva na Hajib wanatakiwa Afrika Kusini na ilishindikana mwaka jana kuhamia huko kwa sababu ya mikataba na klabu zao, lakini kwa kuwa wanaekekea kumaliza kandarasi zao wafukuzie nafasi hizo.
  “Mimi naomba nyinyi Waandishi wa Habari ndiyo muandike sana kuwahamasisha hao vijana waondoke wakakuze uwezo wao Afrika Kusini,”alisema mchezaji huyo wa zamani wa TP Mazembe ya DRC.  
  Kwa sasa Mkude na Hajib ni wachezaji wa Simba SC na Msuva Yanga zote za Dar es Salaam. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AWAKUMBUSHA MKUDE, MSUVA NA HAJIB DILI ZA SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top