• HABARI MPYA

  Monday, April 03, 2017

  TENISI WALEMAVU TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  TIMU ya tenisi ya Taifa yaitaji Msaada kushiriki Mashindano ya Dunia ya BNP Paribas World Team Cup-Wheel Chair Tennis.
  Timu ya Tanzania ya viti vya magurudumu iliyo fauru kushiriki mashindano ya BNP Paribas World Team Cup-Wheel Chair Tennis inaitaji msaada mkubwa, Wito kwa wa Tanzania wote ,Makampuni na watu Binafsi kuiwezesha timu hii kwa hali na mali ili iweze kushiriki kiushindani michuano hiyo ambayo kama itafanikiwa kushinda wataiweka nchi kwenye nafasi nzuri Zaidi ya Tennis.
  BNP Paribas World Team Cup ni mashindano yenye hadhi sawa na Davis Cup na Fed Cup.BNP Paribas World Team Cup inahusissha madaraja ya wanaume, wanawake, quads na wavulana. Mashindano hayo ya BNP Paribas World Team Cup hufanyika kila mwaka kwa nchi tofauti kupokezana uenyeji ,mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 1 May mpaka 7 May 2017 kwenye kisiwa cha pili kwa ukubwa kwenye bahari ya Mediterania Sardinia, Italia.
  Kutoka kushoto kwenda kulia ni Timu ya Tanzania ya Tennis ya Viti vya Magurudumu, Juma Hamisi, Novatus Emmanuel Temba, Kocha Riziki Salum, Voster Issac and Albert John Churi 
  Michuano hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Baia di Conte Hotel yenye viwanja kumi na moja na Alghero Tennis Club yenye viwanja saba.
  Ili uweze kucheza katika mashindano haya makubwa ni lazima ama uwe umeshinda kwenye mashindano mengine makubwa ya kimataifa au uwe umepitia kwenye mchujo wa Mabara ambao umegawanywa katika Mabara manne ya Africa, Asia na Ocenea (Oceania), America na Ulaya, huku kila bara katika katika mchujo huo ikitoa timu moja bora ya kiume na moja bora ya kike.
  Tanzania imefauru kushiriki kwa upande wa wanaume ambapo itakayowakilishwa na wacheza Tennis wanne ambao ni Juma Hamis (19), Novatus Emmanuel TEMBA (21), Albert John Churi(18) na Voster Isaya( 18) .Nafasi hiyo kwa Tanzania ilipatikana baadaya ya kuwatoa Kenya kwa seti 2-1 kwenye fainali za mchujo wa Bara la Afrika michuano iliyofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya,kwenye mashindano yaliyofanyika kuanzia tarehe 16 February na kukamilika tarehe 19 February 2017.
  Kundi la Wanaume kwenye mashindano haya ya Dunia litashindanisha wachezaji kutoka jumla ya mataifa 16 ambayo ni Argentina ,Australia, Belgium, France, Great Britain,Japan,Korea,Rep.,Netherlands,Spain,Sweden,China,Italy,Thailand,Brazil , Poland na Tanzania.
  Morali ya wachezaji wa Tanzania ambao wamepiga kambi ya mazoezi kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es salaam ni ya hali ya juu,Kocha wa Timu hii Ndg.Riziki Salumu anaelezea kuwa kambi yao inakabiliwa na changamoto nyingi za kiufundi na kiuchumi ikiwemo upungufu na ubovu wa vifaa vya mazoezi viti vya magurudumu mipira na raketi za kuchezea ,pia aliongezea kuwa timu ina changamoto ya kuweza kupata fedha zitakazo hakikisha safari yao itakayo gharimu takribani dola za kimarekani 12,000.00.
  Timu inatarajia kuondoka nchini kati ya tarehe 28 na 29 April 2017.Shime kwa wa Tanzania kuisaidia timu hii ili ukifika wakati wa kuwapokea tuwe tumekamilisha haki na wajibu ya kushangilia ushindi wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TENISI WALEMAVU TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top