• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2017

  SIMBA YAWATUMIA SALAMU MBAO, YAWAFUMUA 7-0 GEITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imepoza machungu ya kipigo cha 2-1 kutoka Kagera Sugar Jumapili kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa kirafiki Uwanja wa shule ya Msingi Waja, Geita jioni ya leo.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya viungo Said Hamisi Ndemla, Pastory Athanas, Mwinyi Kazimoto moja kila mmoja wakati Mohammed Ibrahim alifunga mawili sawa na mshambuliaji Muivory Coast, Frederick Blagnon.
  Simba imeweka kambi Geita ikitokea Bukoba, ambako Jumapili ilichapwa 2-1 na wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.
  Na Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu, dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza wiki ijayo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWATUMIA SALAMU MBAO, YAWAFUMUA 7-0 GEITA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top