• HABARI MPYA

  Monday, April 03, 2017

  MALINZI AZIPONGEZA JKT OLJORO, MAWENZI NA TRANSIT CAMP KUPANDA DARAJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amezipongeza timu za JKT Oljoro ya Arusha, Mawenzi ya Morogoro na Transit Camp ya Shinyanga kwa kufanikiwa kupanda daraja baada ya kufanya vema kwenye hatua ya Nne Bora (Play off) iliyofikia kikomo jana Aprili mosi, mwaka huu.
  Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amezitaka timu hizo sasa kujiimarisha katika nyanja za usajili na maandalizi mengine ili kuwa timu za ushindani katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambako watashiriki kuanzia msimu mpya utakaoanza Julai, mwaa huu.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi amezipongeza timu zilizopanda Daraja la Kwanza Tanzania Bara
  “Nichukue nafasi hii kuzipongeza timu zote ambazo zimepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Pili na kwenda Ligi Daraja la Kwanza. Pongezi nyingi ziwaendee wanafamilia wote kuanzia viongozi, wachezaji, waamuzi walioamua mechi zao, mashabiki nakadhalika,” amesema Malinzi na kuongeza:
  “Huu ni uthibitisho kuwa timu zote ziliajianda vya kutosha na kupata matokeo,naamini hata Cosmopolitan nayo ilijiandaa lakini kwa bahati mbaya pointi hazijatosha kwa msimu huu. Ni imani yangu kuwa itapambana msimu ujao na kufanikiwa.”
  Kadhalika Rais Malinzi alizitakia kila la kheri timu zote katika kumaliza msimu na kuanza msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AZIPONGEZA JKT OLJORO, MAWENZI NA TRANSIT CAMP KUPANDA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top