• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2017

  KWESI APPIAH KOCHA MPYA WA GHANA BLACK STARS

  CHAMA cha Soka Ghana  (GFA) kimemteua Nahodha wa zamani wa timu yake ya taifa, James Kwesi Appiah kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Black Stars kwa mara ya pili.
  Appiah, mwenye umri wa miaka 56, ambaye aliifundisha Black Stars kati ya mwaka 2012 na 2014, anachukua nafasi ya Muisraeli Avram Grant, ambaye aliondoka baada ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Februari mwaka nchini Gabon timu ikiambulia nafasi ya nne.
  "Uamuzi umechukuliwa na Kamati Kuu ya GFA Jumanne Aprili 4, 2017 baada ya kuthibitisha taarifa ya Kamati ya watu sita wa kutafuta kocha,".
  "Appiah atapewa mkataba wa miaka miwili na ataanza majukumu haya Mei 1, mwaka 2017. Pia atachukua majukumu kamili ya timu ya wachezaji wa nyumbani ya Black Stars,” imesema taarifa ya GFA.
  Beki huyo wa zamani wa kushoto enzi zake anacheza soka, anasifika kwa Ghana kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
  Pamoja na hayo, akaachia nafasi hiyo kwa maridhiano Septemba 2014 baada ya kiwango kisichoridhisha nchini Brazil.
  Baadaye akajiunga na Al Khartoum ya Sudan na kuifanya timu hiyo kuwa tishio kuanzia nyumbani hadi kwenye michuano ya Afrika.
  Pia alifanya kazi kama Kocha Msaidizi wa Black Stars kuanzia mwaka 2007 hadi 2012.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KWESI APPIAH KOCHA MPYA WA GHANA BLACK STARS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top