• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2017

  BANDA AOMBA RADHI KWA KUMCHAPA KONDE KAVILLA

  Na Mwandishi Wetu, SONGEA
  BEKI wa Simba, Abdi Banda ameomba radhi kwa mashabiki wa soka nchini kwa kitendo chake cha kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Banda alikuwa mwenye bahati kwa kutotolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumtwanga ngumi Kavilla Jumapili katika mchezo ambao Simba ililala 2-1.
  Lakini siku mbili baadaye, Banda ameamua kuvunja ukimya na kuomba radhi kwa kitendo chake hicho.
  “Nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Watanzania na kaka yangu (Kavilla) kwa tukio lilitokea Jumapilim, kwa sababu mimi na yeye ndiyo tunajua kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea,”amesema Banda.  
  Abdi Banda nyuma ya George Kavilla kabla ya mchezo wa Jumapili

  Banda amesema kwamba alikutana na Kavilla baada ya mchezo kumuomba radhi ana kwa ana kwa kitendo kile, lakini ameona haitoshi bali pia awaombe radhi wapenzi wa soka kupitia vyombo vya Habari. 
  Baada ya kunusurika kadi Jumapili, sasa Banda atalazimika kuomba dua na Kamati ya Saa 72 pia isimchukulie hatua. 
  Adhabu yoyote ya kumuweka nje Banda litakuwa pigo kwa Simba katika kipindi hiki cha kumalizia msimu ikiwa inafukuzana na mahasimu, Yanga kwenye mbio za ubingwa.
  Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 55 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 56 za mechi 25 pia.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BANDA AOMBA RADHI KWA KUMCHAPA KONDE KAVILLA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top