• HABARI MPYA

  Thursday, March 09, 2017

  ZANACO KUMKOSA MTU HUYO ANGEKUWEPO YANGA WANGEKOMA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Zanaco FC, Munamba Numba amesema kwamba ana wachezaji wengi wa kuziba pengo la mshambuliaji wake hatari, Fashion Sakala kuelekea mechi na Yanga.
  Zanaco itawasili jioni ya leo tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Na kocha Munamba amesema kwamba amesema anafahamu watamkosa Sakala, waliyemuuza Spartak Moscow ya Urusi, lakini kuna wachezaji wa kutosha wa kuziba pengo lake.
  Fashion Sakala (kulia) hatakuwepo Zanaco ikiivaa Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika

  Zanaco pita itamkosa kipa Mangani Banda ambaye yupo na mshambuliaji Fashion Sakala kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Zambia, Young Chipolopolo kinachocheza fainali za Afrika za Afrika za vijana chini ya umri w miaka 20, ambazo Zambia ni wenyeji.
  Kwa upande wao, Yanga wataendelea kumkosa mshambuliaji wao tegemeo, Mzimbabwe Donald Ngoma kwenye mchezo huo utakaorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Azam anayesumbuliwa na maumivu ya goti.
  Yanga wanaingia kwenye hatua hiyo baada ya kuitoa Ngaya Club de Mde ya Comoro kwa jumla ya mabao matano kwa mawili, ikishinda matano kwa moja mjini Moroni na kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja Dar es Salaam, wakati Zanaco iliitoa APR ya Rwanda kwa bao moja bila, ililoshinda Kigali kufuatia sare ya bila bila mjini Lusaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANACO KUMKOSA MTU HUYO ANGEKUWEPO YANGA WANGEKOMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top