• HABARI MPYA

    Tuesday, March 07, 2017

    YANGA WALALAMIKA KUBADILISHA UWANJA ‘JUU KWA JUU’

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imelalamikia kubadilishiwa Uwanja kutoka wa Taifa hadi Uhuru kwa ajili ya mchezo wao wa leo dhidi ya Kiluvya United.
    Yanga SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi wa kishindo wa mabao 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Na kumbe mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Yanga walijua utachezwa Taifa, lakini TFF ikabadilisha bila kuwashirikisha.
    Pamoja na ushindi wa 6-1 dhidi ya Kiluvya United leo, Yanga wamelalamika kubadilishiwa Uwanja kutoka Taifa hadi Uhuru 

    Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amelalamikia hali hiyo kwani Uwanja wa Uhuru si mzuri katika eneo la kuchezea na huwasababishia maumivu wachezaji.
    Na Mwambusi amesema kwamba wanafanyiwa hivyo wakati Jumamosi watakuwa mchezo mgumu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia.
    “Kitendo cha kutubadilishia Uwanja kwa kweli si kizuri, sisi tulijua tunakwenda kucheza Taifa, kufika tunaambiwa tunacheza Uhuru, athari zake ni kwamba wachezaji wetu wawili wameumia leo,”.
    Mwambusi amewataja wachezaji walioumia ni Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi ambao wanaongeza idadi ya majeruhi Yanga hadi kufika watatu, wakiungana na mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe kuelelea mechi ya kwanza ya hatua ya 32 Bora Ligi ta Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco Jumamosi Dar es Salaam.
    Baada ya ushindi wa leo uliotokana na mabao ya Mzambia Obrey Chirwa aliyefunga manne na Mwashiuya na Mahadhi waliofunga moja kila mmoja, Yanga inarejea kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Zanaco.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WALALAMIKA KUBADILISHA UWANJA ‘JUU KWA JUU’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top