• HABARI MPYA

    Wednesday, March 08, 2017

    YANGA NA ZANACO KIINGILIO POA 3,000

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Zanaco ya Zambia Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa Sh. 3,000.
    Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametaja viingilio vya mchezo huo leo akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online na kwamba VIP A itakuwa Sh. 20,000 na VIP B na C kote mashabiki watakaa kwa Sh. 15,000.
    Mchezo huo utanyeshwa moja kwa na Televisheni ya Azam, jambo ambalo ni faraja kwa mashabiki wa timu hiyo ambao hawataweza kwenda uwanjani, hususan wa nje ya Dar es Salaam.
    Kocha wa Yanga, George Lwandamina atamenyana na timu ya nyumbani Jumamosi 

    Yanga ilifuzu hatua ya 32 Bora ya michuano hiyo, baada ya kuitoa Ngaya Club de Mde ya Comoro kwa jumla ya mabao matano kwa mawili, ikishinda matano kwa moja mjini Moroni na kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja Dar es Salaam, wakati Zanaco iliitoa APR ya Rwanda kwa bao moja bila, ililoshinda Kigali kufuatia sare ya bila bila mjini Lusaka.
    Yanga imeingia kambini leo kwa maandalizi ya mchezo huo baada ua jana kufanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi wa 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana, mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao manne peke yake, huku mengine yakifungwa na viungo Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi. 
    Yanga sasa itamenyana na Prisons katika Robo Fainali Machi 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Robo fainali nyingine zitakuwa kati ya Simba SC na Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA ZANACO KIINGILIO POA 3,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top