• HABARI MPYA

    Friday, March 03, 2017

    TORRES AUNUSURIKA KUFA UWANJANI, AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUANGUKIA KICHWA VIBAYA

    MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana alikimbizwa hospitali nchini Hispania baada ya kuumia kichwani. Torres aliuamia baada ya kuingia dakika ya 65 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Kevin Gameiro.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea, kwanza aliumia mapema tu katika mchezo wa Liga usiku wa jana dhidi ya Deportivo La Coruna Uwanja wa Manispaa ya Riazor mjini La Coruna, timu hizo zikitoka sare ya 1-1.
    Aliangukia kichwa uwanjani baada ya kugongana na Alex Bergantinos na kuwashitua wachezaji wenzake baada ya hali yake kubadilika. Gabi alipigwa na Torres wakati akijaribu kumzuiaa asiueze ulimi.

    Wachezaji wa Atletico Madrid wakijaribu kumzuia Fernando Torres asiumeze ulimi baada ya kuumia jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Hata hivyo, Atletico Madrid imethibitisha mchezaji wake huyo anaendelea vizuri hospital. 
    Katika mchezo huo, Florin Andone alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 13, kabla ya Antoine Griezmann kuisawazishia Atletico dakika ya 68.
    Baadaye Torres mwenyewe akaandika kwenye akaunti yake Twitter kuwaambia mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya hali yake: "Asante nyingi kwa wote kwa kunifuatilia hali yangu na kwa meseji zenu za kunifariji. Ilikuwa ni hofu tu. Natumai kurejea karibuni!,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TORRES AUNUSURIKA KUFA UWANJANI, AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUANGUKIA KICHWA VIBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top