• HABARI MPYA

  Tuesday, March 14, 2017

  SIMBA SC WAPATA MAPOKEZI MAKUBWA ARUSHA

  Na Clement Shari, ARUSHA
  TIMU ya Simba imewasili mjini Arusha jana tayari kabisa kuvaana na wenyeji Madini ya hapa katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Simba SC imetua Arusha Jumatatu wiki hii ikitokea mkoani Dodoma ilipopita kucheza  
  mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma na kufanikiwa kuitandika 3-0.
  Baadaye Simba ikaja Arusha kwa kupitia Manyara, ambako ilipokelewa na mashabiki wa timu hiyo huku winga wa timu hiyo, Shiza Ramadhani Kichuya akipata mapokezi mazuri zaidi.
  Jijini Arusha mashabiki wa timu hiyo walienda kuipokea timu yao katika eneo  
  la Kisongo nje kidogo ya mji ambako misafara ya pikipiki maarufu kama bodaboda na magari ya  
  kawaida ilipamba mapokezi hayo.
  Kwa upande wao, Chama cha Soka Arusha (ARFA), kimesema maandalizi yote  
  kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri. Katibu wa ARFA, Zakayo Mjema amesema kwa sasa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umefungwa ili kwa ukarabati wa hapa na pale ikiwa ni pamoja na sehemu ya kuchezea. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPATA MAPOKEZI MAKUBWA ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top