• HABARI MPYA

  Thursday, March 09, 2017

  SIMBA NA MADINI YASOGEZWA MBELE, YANGA KUPANGIWA TAREHE MPYA KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Machi 19.
  Taarifa ya TFF leo imesema kwamba Robo Fainali mbili za kwanza za ASFC zitachezwa Machi 18 na 19, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti.
  Mechi hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera wakati siku inayofuata Machi 19 Simba itacheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
  Awali Simba ilikuwa icheze Machi 18, mwaka huu, lakini siku hiyo uwanja huo utakuwa na shughuli za kijamii hivyo sasa utachezwa siku ya Jumapili Machi 19, mwaka huu.
  Mechi nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye. 
  Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Yanga dhidi ya Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.
  Pia bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA MADINI YASOGEZWA MBELE, YANGA KUPANGIWA TAREHE MPYA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top