• HABARI MPYA

  Friday, March 17, 2017

  SAMATTA AMFUATA MOURINHO ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atacheza Robo Fainali ya UEFA Europa League baada ya timu yake kufuzu licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KAA Gent usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Kwa matokeo hayo, Genk inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-3, baada ya awaoi kushinda 5-2 ugenini wiki iliyopita kwenye mchezo wa kwanza wa 16 Bora ikiungana na vigogo wengine wa Ulaya, wakiwemo Manchester United ya England ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
  Genk walitangulia kwa bao la Timothy Castagne dakika ta 20 jana, kabla ya Louis Verstraete kuisawazishia Genyt dakika ya 83.
  Mchezo wa jana umekuwa wa 49 kwa Samatta akiwa amefunga mabao 17 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC.
  Mechi 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 31 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 30 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 30 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tisa msimu huu na katika mabao hayo 17, 11 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen/Janssens dk80, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Schrijvers dk45, Buffel/Trossard dk72, Boetius na Samatta.
  KAA Gent : Kalinic, Gigot, Coulibaly, Mitrovic, Kalu, Dejaegere, Perbet/Verstraete dk61, Simon, De Smet, Foket na Rabiu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AMFUATA MOURINHO ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top