• HABARI MPYA

  Wednesday, March 08, 2017

  ROONEY AACHWA MAN UNITED SAFARI YA URUSI

  Wayne Rooney akiendesha gari lake viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Carrington jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Kikosi cha Man United kilichokwenda Rostov  

  De Gea, Romero, O'Hara; Valencia, Jones, Rojo, Smalling, Blind, Darmian, Young; Carrick, Herrera, Fellaini, Pogba, Mata, Lingard, Mkhitaryan; Martial, Rashford, Ibrahimovic. 
  NAHODHA Wayne Rooney hajajumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United kilichokwenda Urusi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa UEFA Europa League dhidi ya wenyeji, Rostov.
  Mshambuliaji huyo wa Mashetani hao Wekundu hayumo kwenye kikosi cha wachezaji 20 kilichoondoka jana Uwanja wa ndege wa Manchester kwa ajili ya mechi na Rostov-on-Don kusini magharibi mwa Urusi.
  Rooney anaweza kuhitajika wakati United inacheza na Chelsea kwenye Robo Fainali ya Kombe la FA Jumatatu, kwa sababu Zlatan Ibrahimovic amekubali adhabu ya kufungiwa mechi tatu kufuatia kumpiga kiwiko mchezaji wa Bournemouth, Tyrone Mings mwishoni mwa wiki.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROONEY AACHWA MAN UNITED SAFARI YA URUSI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top