• HABARI MPYA

    Wednesday, March 08, 2017

    MWANJALI SASA LABDA MWEZI UJAO KUREJEA SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    BEKI wa kati tegemeo wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali ataendelea kuwa nje kwa mwezi wote wa Machi kutokana na maumivu ya goti.
    Mwanjali hajajumuishwa kwenye kikosi kinachoondoka asuhuhi ya kesho Dar es Salaam kwenda ziara ya Dodoma kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Polisi Jumamosi wiki hii Uwanja wa Jamhuri mjini humo.
    Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kwamba Mwanjali hatakwenda Dodoma na hatahusishwa kwenye programu yoyote ya timu mwezi huu wa Machi.

    Method Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11 

    Gembe amesema kwamba wanataka Mwanjali aendelee kupatiwa matibabu hadi awe fiti kabisa, ili akirejea iwe amerudi rasmi kuisaidia timu.
    “Tunataka apone vizuri kabisa ndiyo arejee uwanjani. Kwa hiyo Machi yote hatakuwemo kwenye programu za timu,”amesema Gembe. 
    Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ikishinda 3-0.
    Mwanjali aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC, alitolewa kwa machela siku hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Mwinyi Kazimoto dakika ya 62.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANJALI SASA LABDA MWEZI UJAO KUREJEA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top