• HABARI MPYA

  Friday, March 10, 2017

  MLANDIZI QUEENS WALIVYOKABIDHIWA UMALKIA WA SOKA YA WANAWAKE TANZANIA LEO

  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, Nahodha wa Mlandizi Queens, Mwanahamisi Omar 'Gaucho' baada ya kumaliza na pointi 15 za mechi tano katika Sita Bora ya michuano hiyo na kuwapiku JKT Queens waliomaliza na pointi 12
  Mwanahamisi Gaucho akiinua Kombe la Ligi Kuu ya Wanawake leo baada ya kuiongoza Mlandizi Queens kuifunga 5-0 Panama ya Iringa leo akifunga mabao manne
  Rais Jamal Malinzi akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh Milioni 5 baada ya ubingwa
  Jamal Malinzi akimvalisha Medali Mwenyekiti wa Chama cha Soka Pwani (COREFA), Hassan Hassanoo kufuatia mafanikio ya Mlandizi Queens
  Meneja wa Idara ya Michezo ya Azam TV, Baruwan Muhuza (kulia) akimvalisha Medali mchezaji wa JKT Queens iliyomaliza nafasi ya pili, Fatuma Issa 'Foe'
  Wachezaji wa Mlandizi Queens wakisherehekea na Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MLANDIZI QUEENS WALIVYOKABIDHIWA UMALKIA WA SOKA YA WANAWAKE TANZANIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top