• HABARI MPYA

  Tuesday, March 14, 2017

  MAYWEATHER AREJEA ULINGONI RASMI, KUZIPIGA NA MCGREGOR JUNI 10 LAS VEGAS

  WABABE Floyd Mayweather na Conor McGregor watapigana Juni 10, mwaka huu.
  Mmarekani anayefahamika kama Money na Muireland aitwaye Notorious wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa shehemu. ya pambano lao.
  Kila mmoja ametaja bei yake ya kupandia ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100, ingawa kiuhalisia McGregor atatakiwa kushusha bei ili kuhamishia ujuzi wake wa UFC katika ndondi. 
  Mayweather amesema kwamba rasmi amerejea ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, legendary Rocky Marciano na hilo litaitwa "Pambano la Karne".
  Floyd Mayweather atapanda ulingoni Juni 10, mwaka huu ukumbi wa T-Mobile Arena kupigana na Conor McGregor PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER AREJEA ULINGONI RASMI, KUZIPIGA NA MCGREGOR JUNI 10 LAS VEGAS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top