• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2017

  MALI HATARINI KUONDOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018

  TIMU ya taifa ya Mali inaweza kuondolewa kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 baada ya Serikali kuwafukuza viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo.
  Washika mkia hao Afrika Magharibi wanatarajiwa kucheza na Morocco mara mbili, vinara wa kundi Ivory Coast na Gabon mwaka huu.
  Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) halizipi mamlaka Serikali kuingilia mchezo huo na imeshuhudiwa nchi nyingi za Afrika zikifungiwa kwa sababu hiyo.
  "Uamuzi wa Wizara unakwenda kinyume na uhuru wa vyama vya soka,"imesema taarifa ya FIFA.
  "Iwapo uamuzi huo hautakuwa umevatilishwa hadi Ijumaa (juzi), Machi 10, moja kwa moja kesi hiyo titawasilishwa FIFA katika idara husika,".
  Pamoja na tishio hilo, Wizara ya Michezo ya Malia iliendelea kushikilia msimamo wake hadi jana.
  "Ni uamuzi wa Serikali na hautabadilika," alisema Waziri wa Michezo, Mwanasheria Amadou Diarra Yalcouye na kuongeza; "FIFA haiwezi kuifanya serikali ibadili uamuzi huu. Muda si mrefu Wizara itaaunda Kamati ya Muda ya kuendesha na kuiunganisha familia ya soka,".
  Mali ilivurunda katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon, ikifunga bao moja tu wakifungwa na Ghana na kutoa sare na Misri na Uganda.
  Kwa sasa nchi hiyo inashika nafasi ya 61 katika viwango vya ubora wa soka vya FIFA na namba 12 kwa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALI HATARINI KUONDOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top