• HABARI MPYA

  Thursday, March 09, 2017

  MAAJABU MENGINE BARCA ILIWAHI KUFANYA KABLA YA JANA...

  TIMU ya Barcelona jana imeitoa PSG katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa 6-1 usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou kwenye mchezo wa marudiano. 
  Hilo halikutarajiwa baada ya Barca kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza mjini Paris. Mabao ya Barca jana yalifungwa na Luis Suarez dakika ya tatu, Layvin Kurzawa aliyejifunga dakika ya 40, Lionel Messi kwa penalti dakika ya 50 baada ya Neymar ambaye pia alifunga mawili dakika za 88 na 90 kwa penalti kuangushwa na Sergi Roberto dakika ya 90 na ushei wakati la PSG lilifungwa na Edinson Cavani dakika ya 62. 
  Je, unajua ushindi huo chini ya kocha Luis Enrique ambaye tayari amesema ataondoka mwishoni mwa msimu ni wa ngapi kwa ukubwa nyumbani kwa Barca?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAAJABU MENGINE BARCA ILIWAHI KUFANYA KABLA YA JANA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top