• HABARI MPYA

  Saturday, March 11, 2017

  LWANDAMINA AWAPANGA PAMOJA NGOMA, KAMUSOKO, CHIRWA NA MSUVA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM 
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina ameanzisha kikosi cha muunganiko mzuri kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Lwandamina leo amewarejesha Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma ambao walikuwa majeruhi.
  Kutoka kulia Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Simon Msuva wote wanaanza leo

  Amekuja na safu kali ya ushambuliaji ikiundwa na Ngoma na Mzambia mwenzake, Chirwa.
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Justine Zulu, Donald Ngoma na Obrey Chirwa.
  Katika benchi wapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Justine Zullu, Geoffrey Mwashuya, Oscar Joshua, Juma Mahadhi na Said Juma ‘Makapu’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWAPANGA PAMOJA NGOMA, KAMUSOKO, CHIRWA NA MSUVA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top