• HABARI MPYA

    Thursday, March 09, 2017

    KILA KITU KIPO TAYARI AZAM NA MBABANE, YANGA NA ZANACO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAANDALIZI ya michezo ya kwanza ya hatua ya 32 Bora michuano ya Afrika kati ya wenyeji Yanga na Azam za Tanzania dhidi ya Zacano ya Zambia na Mbabane Swallows ya Swaziland yamekamilika.
    Yanga itakuwa mwenyeji wa Zanaco Jumamosi Uwanja wa Taifa, katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC wataikaribisha Mbabane Swallows Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Waamuzi wa mechi hiyo wanatarajiwa kuwawili leo kutoka Djibouti Djamal Aden Abdi atakayepuliza kipyenga akiasaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime wakaopeperusha vibendera na refa wa akiba mezani Souleiman Djamal. Kamisaa wao katika mchezo huo namba 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
    Viingilio katika mchezo huo kvinatarajiwa kuwa Sh 20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi ya chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.
    Waamuzi wa mechi ya Azam wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa kati, Addissa Abdul Ligali na wasaidizi ni Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina huku Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.
    Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP, Jukwa Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.
    Wakati huohuo, tiketi za waamuzi wa Tanzania walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000 ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata tiketi zao za kusafiri.
    Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Hery Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA KITU KIPO TAYARI AZAM NA MBABANE, YANGA NA ZANACO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top