• HABARI MPYA

    Friday, March 10, 2017

    KAMATI YA NIDHAMU YAIAGIZA TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeagiza sekretarieti yake kutoa wito mwingine kwa wanafamilia watatu wa Chama cha Soka Rukwa (RUREFA) walioshitakiwa mbele ya kamati hiyo.
    Walioshitakiwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ni Mwenyekiti wa RUREFA, Blassy Kiondo; Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, James Makwinya na Kaimu Katibu Mkuu wa RUREFA, Ayoub Nyaulingo.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi
    Madai dhidi ya wanafamilia hao wa mpira wa miguu ni kudharau maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ya kuwataka wasimamishe mchakato wa uchaguzi wa Mkoa mpaka rufaa zilizowasilishwa TFF zitakaposikilizwa.
    TFF ilipeleka mwito wa kuwataka watuhumiwa hao kwenda kujibu madai hayo mbele ya Kamati ya Nidhamu, Machi 8, mwaka huu lakini watuhumiwa hawakutokea kwa sababu mbalimbali.
    Lakini Kamati kwa kuzingatia kanuni ya Nidhamu iliona ni vyema watuhumiwa wakapata nafasi tena ya kuja kujitetea mbele ya kamati hiyo na kama ikitokea wameshindwa kufika, basi watume wawakilishi wao au utetezi kwa njia ya maandishi katika kikao kingine kitakachofanyika Machi 15, mwaka huu saa 12.00 jioni kama barua inavyojieleza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMATI YA NIDHAMU YAIAGIZA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top