• HABARI MPYA

  Tuesday, March 14, 2017

  HASSAN KABUNDA NDIYE MCHEZAJI BORA WA FEBRUARI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji wa Mwadui FC, Hassan Salum Kabunda ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari, mwaka huu.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Kabunda amewapiku washambuliaji wa Simba, Mrundi Laudit Mavugo na mzalendo Ibrahim Hajibu baada ya mechi mechi tatu za Februari kushinda tuzo hiyo.
  Hassan Salum Kabunda ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari, mwaka huu

  “Kabunda amecheza dakika 270 katika mechi tatu ambazo Mwadui wameshinda mbili na kupoteza mechi moja, hivyo kujikusanyia pointi 6 na kupanda kutoka nafasi ya nane hadi ya sita,”amesema Mapunda.
  Aidha, Ofisa huyo wa TFF amesema mtoto huyo wa beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Kabunda enzi zake akiitwa Ninja au Msudan, katika mechi hizo tatu alifunga mabao manne kati ya sita ambayo Mwadui ilifunga.
  Na kwa ushindi huo, Kabunda atazawadia Sh. Milioni 1 na wadhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HASSAN KABUNDA NDIYE MCHEZAJI BORA WA FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top