• HABARI MPYA

    Friday, March 10, 2017

    FARID AANZA KUANDALIWA KUCHEZA SEGUNDA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Malik Mussa ameanza kutayarishwa kuchezea kikosi cha kwanza cha Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Hispania, maarufu kama Segunda.
    Farid ameanza kupangwa katika mechi za kikosi cha wachezaji wa akina wa Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Hispania, maarufu kama Segunda.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, mwishoni mwa wiki alicheza mechi dhidi ya Real Mallorca ndani ya vikosi vya wachezaji wa akiba wa timu hizo. 
    Hatua hiyo inafuatia Farid kupandishwa kikosi cha kwanza cha Deportivo baada ya kuchezea kikosi cha pili tangu Januari mwaka huu.
    Farid Mussa ameanza kutayarishwa kuchezea kikosi cha kwanza cha Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi ya Segunda

    “Ninamshukuru Mungu kwa kweli ninaendelea vizuri, baada ya kupandishwa kikosi cha kwanza sasa nimeanza kucheza mechi za kikosi cha wachezaji wa akiba. Sasa ninaendelea kupambana nianze kupata nafasi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza hapa,”amesema Farid.
    Farid alijiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary Desemba mwaka jana kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam. 
    Azam FC ilimtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.
    Farid alitua Hispania kwa mara ya kwanza Aprili 21, mwaka jana baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
    Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo Desemba, 2016.
    Na baada ya kutua Tenerife akapangiwa kuanza kuchezea kikosi cha U-20 ili kupata uzoefu kabla ya wiki iliyopita kupandishwa kikosi cha kwanza kinachocheza Segunda, Ligi ya pili kwa ukubwa Hispania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FARID AANZA KUANDALIWA KUCHEZA SEGUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top