• HABARI MPYA

    Monday, March 13, 2017

    DEGE LA KENYA KUWAPELEKA YANGA ZAMBIA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Yanga SC kitaondoka Dar es Salaam Alhamisi wiki hii kwa ndege ya Shirika la Kenya kwenda Lusaka, Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki. 
    Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo katika mazungumzo na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba msafara huo utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi kadhaa ambao watatajwa baadaye. 
    Yanga imeanza mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa marudiano, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na mabingwa hao wa Zambia katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika mchezo wa juzi, uliochezeshwa na maarefa kutoka Djibouti, Djamal Aden Abdi aliyeyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime, Yanga walitangulia kwa bao winga wake machachari, Simon Happygod Msuva dakika ya 39, kabla ya Zanaco kusawazisha dakika ya 78  kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame.
    Yanga sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini katika mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki ili kusonga mbele hatua ya makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEGE LA KENYA KUWAPELEKA YANGA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top