• HABARI MPYA

    Thursday, March 09, 2017

    CHIRWA AMPONZA REFA AFUTWA KABISA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa refa wa kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
    Hatua hiyo imefikiwa baada ya utetezi wa Simba kudai kwamba hakuona tukio la mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.
    Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao Yanga walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.
    Ahmada Simba alilikataa bao safi la Obrey Chirwa na kumuonyesha kadi ya njano 

    Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
    Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
    Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza, kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo ulisababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo mmoja. Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.
    Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa ni kuipiga faini Yanga Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
    Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Yanga Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHIRWA AMPONZA REFA AFUTWA KABISA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top