• HABARI MPYA

  Monday, March 13, 2017

  CANNAVARO: TUNAWAFUNGA ZANACO KWAO MAPEMA KABISA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba wana uwezo wa kuwafunga Zanaco kwao na kusonga mbele hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Yanga SC ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Matokeo yanamaanisha Yanga watahitaji ushindi wa ugenini katika mchezo wa marudiano nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
  Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema wanaweza kuifunga Zanaco kwao na kusonga mbele hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

  Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online, Cannavaro alisema kwamba hawajakata tamaa kwa sababu wanajua wana nafasi kubwa ya kushinda ugenini.
  “Wapinzani wetu walitumia nguvu nyingi katika mchezo wa ugenini. Na sidhani kama kuna kitu waliacha, sisi tuna mengi tuliacha kwa ajili ya mchezo wa marudiano kwa sababu tayari tuna uzoefu mkubwa wa haya mashindano,”alisema.
  Cannavaro alisema wataitumia wiki hii kwa maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wa marudiano nchini Zambia ili wawatoe Zanaco.  
  Katika mchezo wa juzi, uliochezeshwa na maarefa kutoka Djibouti, Djamal Aden Abdi aliyeyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime, Yanga walitangulia kwa bao winga wake machachari, Simon Happygod Msuva dakika ya 39, kabla ya Zanaco kusawazisha dakika ya 78  kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CANNAVARO: TUNAWAFUNGA ZANACO KWAO MAPEMA KABISA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top