• HABARI MPYA

  Tuesday, March 14, 2017

  BLAGNON AREJEA SIMBA BAADA YA MPANGO WA KUCHEZA KWA MKOPO OMAN KUBUMA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Muivory Coast, Frederick Blagnon amerejea Simba SC baada ya mpango wa kujiunga na Oman Club ya Oman kwa mkopo kushindikana.
  Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Blagnon amerudi baada ya Oman Club kuchelewa kukamilisha taratibu za kumsajili kwa mkopo.
  “Wao (Oman Club) walimuomba huyu mchezaji kwa mkopo, lakini kwa bahati mbaya wakachelewa kukamilisha taratibu za kupata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC),”amesema Kaburu.
  Frederick Blagnon amerejea Simba SC baada ya mpango wa kujiunga na Oman Club kwa mkopo kushindikana

  Kwa sababu hiyo, Kaburu amesema kwamba Blagnon anarejea katika klabu yake, Simba SC na ataendelea kucheza.  Blagnon alijiunga na Simba SC kwa dau la Sh. Milioni 100 kutoka African Sports ya kwao, Ivory Cioats Julai mwaka jana.
  Na baada ya jaribio la kuhamia Oman kwa mkopo kushindikana, anarejea kuungana na wachezaji wengine sita wa kigeni, Waghana, kipa Daniel Agyei na kioungo James Kotei, mabeki Mkongo Janvier Bokugu, Mganda Juuko Murshid na Mzimbabwe Method Mwanjali na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kukamilisha idadi ya wachezaji saba kwa mujinu wa kanuni.  
  Blagnon tayari amejiunga na kambi ya Simba Arusha ambako Jumapili kitamenyana na wenyeji, Madini FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BLAGNON AREJEA SIMBA BAADA YA MPANGO WA KUCHEZA KWA MKOPO OMAN KUBUMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top