• HABARI MPYA

  Friday, February 10, 2017

  ZIMAMOTO TAYARI KUWAKABILI FERROVIARIO KESHO LIGI YA MABINGWA ZANZIBAR

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Zanzibar katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Zimamoto kesho wanatupa kete yao ya kwanza katika michuano hiyo, watakapomenyana na Ferroviario da Beira ya Msumbiji.
  Mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali utafanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ally Cheupe ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekamilika yote na wageni, Ferroviario wapo visiwani humo tangu jana.
  “Tunatoka kwenye kikao cha kabla ya mechi hapa, kimesisha salama na kwa ujumla maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kiasi cha kutosha,”alisema Cheupe. 
  Kwa upande wake, kocha wa Zimamoto Seif Bausi alisema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo baada ya maandalizi ya kutosha.
  “Tumekuwa na kipindi kizuri cha maandalizi na cha kutosha kabla ya mchezo huo. Na ninapenda kuwahakikishia wapenzi wa soka visiwani hapa kwamba tuko tayari kwa mchezo,”alisema.
  Katika mchezo wa kesho, Zimamoto itawategemea washambuliaji wake wawili hatari, Ibrahim Hilika anayeongoza kwa mabao yake 13 kwenye Ligi Kuu ya Zanzibar na Hakim Khamisi ‘Man’ anayefuatia kwa mabao yake 10.
  Baada ya kipute cha kesho, keshokutwa nyasi za Uwanja wa Amaan, Zanzibar zitawaka tena moto kwa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya KVZ na Messager Ngozi ya Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIMAMOTO TAYARI KUWAKABILI FERROVIARIO KESHO LIGI YA MABINGWA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top