• HABARI MPYA

    Saturday, February 18, 2017

    YANGA YALAZIMISHWA SARE NA WACOMORO, LAKINI YASONGA MBELE AFRIKA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imefuzu raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ngaya Club de Mde ya Comoro jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga inafuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2, baada ya Jumapili iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro.
    Mchezo huo uliochezeshwa na marefa Alex Muhabi, washika vibendera Ronald Katenya na Lee Okello hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
    Wachezaji wa Yanga wakimpongza mfungaji wa bao lao, Mwinyi Hajji Mngwali
    Obrey Chirwa wa Yanga akipiga kichwa ambacho kilikwenda nje ya lango la Ngaya
    Simon Msuva akimiliki mpira mbele ya beki wa Ngaya
    Beki wa Yanga, Vincent Bossou akipiga kichwa mbele ya mchezaji wa Ngaya
    Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke akimtoka mchezaji wa Ngaya leo

    Na Ngaya ndiyo waliokuwa wa kwanza kuepata bao dakika ya 19 kupitia kwa Zahir Mohammed aliyefumua shuti na mpira ukambabatiza Vincent Bossou kichwani na kumpita kipa namba moja Tanzania, Deo Munishi ‘Dida’.
    Yanga ilisawazisha bao hilo dakika ya 43 kupitia kwa beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, aliyefumua shuti kali kutoka umbali wa mita 25, baada ya pasi ya Kevin Yondan.
    Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na kosa kosa zikawa za pande zote mbili.
    Lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na kwa matokeo hayo, Yanga sasa itamenyana na Zanaco ya Zambia, ambayo imeitoa APR ya Rwanda. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Hassan Kessy dk71, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke/Said Juma 'Makapu' dk72, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin/Mahadhi dk59.
    Ngaya SC; Said Mmadi, Said Hachim, Chadhuili Mradabi, Said Anfane, Franck Said Abderemane, Youssouf Ibrahim Moidjie, Rakotoarimanana Falinirino/Chabane Saandi Youddouf dk70, Berthe Alpha, Zamir Mohammed/Kadafi Said Mze dk57, Mounir Moussa na Said Toihir.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YALAZIMISHWA SARE NA WACOMORO, LAKINI YASONGA MBELE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top