• HABARI MPYA

  Wednesday, February 15, 2017

  WAGANDA KUCHEZESHA YANGA NA NGAYA JUMAMOSI TAIFA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MAREFA kutoka Uganda watachezesha mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Ngaya Club de Mde ya Comoro Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na washika vibendera Ronald Kakenya na Lee Okello.
  Refa wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.
  Yanga ilishinda mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza Jumapili mjini Moroni Comoro na wanatarajiwa kuwa na mteremko katika mchezo huo wa marudiano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAGANDA KUCHEZESHA YANGA NA NGAYA JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top