• HABARI MPYA

  Friday, February 03, 2017

  SIMBA HAITAKI KURUDIA MAKOSA KWA MAJI MAJI KESHO SONGEA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Simba SC, Jonas Mkude amesema kwamba watajitahidi kesho wasirudie makosa katika mchezo wao dhidi ya Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Simba SC watakuwa wageni wa Maji Maji kesho Uwanja wa Maji Maji mjini Songea wakitoka kufungwa 1-0 na Azam FC Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wao uliopita.
  Na kuelekea mchezo wa kesho, Mkude aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba wachezaji wote wamekubaliana kwenda kupigana kiume ili washinde dhidi ya Maji Maji.
  “Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu dhidi ya wenyeji wetu, kwa sababu kwanza wao watakuwa wanacheza kwao, lakini tumekubaliana kupigana kwa nguvu zetu zetu ili tushinde hii mechi,”alisema.
  Mkude alisema kwamba makosa yaliyotokea kwenye mchezo na Azam hadi wakapoteza kwa kufungwa 1-0 bao pekee na Nahodha John Bocco yaamekwishafanyiwa kazi na kesho mambo yatakuwa tofauti.
  Alisema wanatambua changamoto ya kucheza kwenye Uwanja mbaya kesho, lakini wamejipanga kikamilifu kwa namna yoyote washinde mchezo huo.
  “Uwanja wa Maji Maji unajulikana sio mzuri, lakini sisi kwa kuwa tulijua tunakuja huku tulijiandaa vizuri kucheza katika mazingira haya,”alisema Nahodha huyo ambauye hucheza nafasi ya kiungo Simba SC.
  Baada ya kufungwa na Azam 1-0, Simba imeangukia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu sasa ikizidiwa kwa pointi moja na Yanga SC, (46-45) baada ya kila timu kucheza mechi 20.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA HAITAKI KURUDIA MAKOSA KWA MAJI MAJI KESHO SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top