• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2017

  SIASIA APEWA NAFASI KUBWA YA KUWA KOCHA MPYA WA RWANDA

  SHIRIKISHO la Soka Rwanda (FERWAFA) limetangaza orodha fupi ya watu wanane wanaowani nafasi ya ukocha wa timu yake ya taifa ya wakubwa, Amavubi ambayo imeachwa wazi na Johnny McKinstry wa Ireland Kaskazini.
  Mnigeria Samson Siasia, ambaye aliiongoza Dream Team kutwaa Medali ya Shaba katika Olimpiki ya Rio 2016 nchini Brazil ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kupewa kibaruwa hicho kati ya hao wanane.
  Mbelgiji Georges Leekens, ambaye alijiuzuku ukocha wa Algeria mwezi uliopita baada ya kushindwa kuwavusha Desert Foxes nje ya hatua ya makundi, pamoja na kocha wa zamani wa Burkina Faso na Jordan, Paul Put wapo kwenye orodha hiyo pia.
  Wengine wanaoomba nafasi ya ukocha wa Amavubi ni pamoja na kocha wa Botswana, Peter Butler, ambaye bado anaendelea na kazi Zebras, Raoul Savoy, Jose Rui Lopes Aguas, Antoine Hey na Winfried Schafer.
  Rais wa FERWAFA, Vincent Degaule Nzamwita alisema: “Tunataka kuteua kocha ambaye atatupeleka katika kiwango kingine,".
  Kocha mpya atakayeteuliwa ataiandaa Amavubi kwa ajili ya mechi ya kufuzu CHAN ya 2018, ambayo Rwanda itaanza na Tanzania mechi ya kwanza ikichezwa Julai 14-16 mjini Dar es Salaam kabla ya marudiano wiki inayofuata mjini Kigali.
  Rwanda pia imepangwa Kundi H kwenye mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 pamoja na Ivory Coast, Guinea na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  Mnigeria Samson Siasia anaopewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mpya wa Rwanda 

  ORODHA YA WANAOWANIA UKOCHA WA RWANDA;
  1. Antoine Hey (Ujerumani)
  2. Georges Leekens (Ubelgiji)
  3. Jose Rui Lopes Aguas (Ureno)
  4. Paul Put (Ubelgiji)
  5. Peter James Butler (England)
  6. Winfried Schafer (Ujerumani)
  7. Raoul Savoy (Uswisi)
  8. Samson Siasia (Nigeria)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIASIA APEWA NAFASI KUBWA YA KUWA KOCHA MPYA WA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top