• HABARI MPYA

    Saturday, February 04, 2017

    SERENGETI BOYS YAPANGWA KUNDI B GABON

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imepangwa Kundi B pamoja na Angola, Mali na Niger katika fainali za vijana chini ya umri wa miaka (AFCON U-17) mwaka huu Gabon.
    Katika makundi yaliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wenyeji Gabon watakuwa Kundi A pamoja na Guinea, Cameroon na Ghana na michuano hiyo itaanza Aprili 2 mwaka huu.
    Tanzania imerejeshwa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kongo Brazzaville iliyotumia mchezaji aliyezidi umri.
    Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwapa siku 10 Shirikisho la Soka Kongo (FECOFOOT) kumuwasilisha mchezaji Langa Lesse Bercy mjini Libreville, Gabon afanyiwe vipimo vya MRI ili kuthibitisha umri wake kama anaruhusiwa kucheza mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, lakini wameshindwa kufanya hivyo.
    Na hiyo ilikuwa mara ya tatu, FECOFOOT wanashindwa kumpeleka Langa Lesse Bercy akafanyiwe vipimo baada ya kushindwa kufany hivyo awali mara mbili mjini Cairo, Misri kwa vipimo.
    Fainali za U-17 Afrika ilikuwa zifanyike nchini Madagascar kuanzia Aprili mwaka huu, lakini mwezi uliopita CAF iliivua uenyeji na kutoa muda hadi Januari 30 mwaka huu nchi nyingine kujitokeza kuomba uenyeji kabla ya juzi kuiteua Gabon kuandaa fainali hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAPANGWA KUNDI B GABON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top