• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2017

  SAMATTA AGONGA ZOTE 90, GENK YALAZIMISHA SARE UGENINI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 2-2 ugenini dhidi ya wenyeji, Astra Uwanja wa Marin Anastasovici mjini Giurgiu, Romania katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Europa League.
  Matokeo hayo ni mwanzo mzuri kwa Genk katika hatua hii, kwani sasa watatakiwa kushinda hata 1-0, au kutoa sare ya 0-0 nyumbani ili kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya.
  Mbwana Samatta akitoka uwanjani baada ya mchezo wa jana ambao alidhibitiwa vikali na kushindwa kufunga

  Mabao ya Genk jana yalifungwa na Timothy Castagne dakika ya 25 na Leandro Trossard dakika ya 83, wakati ya Astra yalifungwa na Constantin Valentin Budescu dakika ya 43 na Takayuki Seto dakika ya 90.
  Jana Samatta alicheza mechi ya 42 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 24 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 23 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 13 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Heynen, Kumordzi/Berge DK65, Pozuelo/Boetius dk76, Trossard/Buffalo dk88, Writers na Samatta.
  FC Astra Giurgiu : Lung, Alves, Fabricio, Seto, Budescu, Morais, Niculae/Florea dk65, Sapunaru, Ionita/Bus dk65/Nicoara dk81, Stan na Teixeira.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AGONGA ZOTE 90, GENK YALAZIMISHA SARE UGENINI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top