• HABARI MPYA

    Saturday, February 11, 2017

    SAMATTA APIGA BAO MECHI YA MAHASIMU, GENK YAUA 3-0

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amerejea uwanjani usiku wa jana na kuifungia KRC Genk bao la pili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu, Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Uwanja wa Stayen, Sint-Truiden, St.-Trond.
    Samatta aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu aumie mgongo Februari 1, alifunga bao lake dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo fundi wa Kispaniola, Alejandro Pozuelo Melero. 
    Na Pozuelo alimsetia Samatta kufunga bao la pili, akitoka kufunga bao la kwanza yeye mwenyewe dakika ya 37, akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji chipukizi Mbelgiji, Siebe Schrijvers.
    Mbwana Samatta akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao lake jana

    Bao la tatu la KRC Genk ambayo sasa inafikisha pointi 41 katika nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 26, lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 45. 
    Februari 1 Samatta alicheza kwa dakika 23 tu kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akiiacha KRC Genk ikifungwa 1-0 na KV Oostende Uwanja Luminus Arena, Genk katika mchezo wa Kombe la Ubelgiji na kutolewa.
    Jana Samatta alicheza mechi ya 41 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 23 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 22 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 11 msimu huu.
    Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
    Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Uronen, Colley/Wouters dk82, Brabec, Castagne, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Boetius dk62 Trossard/Naranjo dk70, Writers na Samatta.
    STVV:Pirard, Mechele, Peeters, Gerkens, Bagayoko/Dussaut dk63, Janssens/Boli dk45, Kotysch, Valdivia, Fernandes, Vetokele na Bolingoli/Ceballos dk45.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA APIGA BAO MECHI YA MAHASIMU, GENK YAUA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top