• HABARI MPYA

  Tuesday, February 14, 2017

  RED ARROWS WAWASILI DAR KUIVAA AZAM KESHO CHAMAZI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kirafiki kati ya Azam na Red Arrows ya Zambia unatarajiwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Azam, Jaffari Iddi amesema kwamba timu imeshaingia kambini tangu jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya timu ya Jeshi la Anga Zambia.    
  Aidha, Jaffar alisema kwamba wageni, Red Arrows nao wamekwishawasili mjini Dar es Salaam na wapo tayari kabisa kwa mchezo huo kesho.
  Jaffar Iddi (kushoto) katika mkutano na Waandishi wa Habari leo

  "Timu imeingia kambini tangu jana na mchezo huu kwetu ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, tunaamini utamsaidia mwalimu kujua timu imefikia wapi na ina mapungufu gani,”alisema.
  Kwa Azam FC huu ni mchezo wa pili wa kimataifa ndani ya wiki mbili, baada ya mapema mwezi huu kucheza na mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na kutoa sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RED ARROWS WAWASILI DAR KUIVAA AZAM KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top