• HABARI MPYA

  Saturday, February 11, 2017

  OMOG AWAANZISHA WOTE, HAJIB, MAVUGO NA LUIZIO DHIDI YA PRISONS LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  KOCHA wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog na leo amewaanzisha wote Juma Luizio, Ibrahim Hajib na Mrundi, Laudit Mavugo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya.
  Na hiyo inafuatia kuwapanga pamoja wote katika mchezo dhidi ya Maji Maji Songea Jumamosi iliyopita na wakaiwezesha Simba SC kushinda 3-0 katika mchezo huo wa Ligi Kuu.
  Kwa ujumla, Omog hajafanya mabadiliko makubwa sana kutoka kikosi kilichoifunga Maji Maji 3-0 Jumamosi iliyopita. 
  Joseph Omog amepanga 'kikosi kazi' mechi na Prisons ya Mbeya leo Uwanja wa Taifa

  Kikosi kinachoanza Simba leo; Daniel Agyei, Janvier Bokongu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib na Juma Luizio.
  Benchi; Peter Manyika, Vincent Costa, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya, Hija Ugando na Pastory Athanas.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AWAANZISHA WOTE, HAJIB, MAVUGO NA LUIZIO DHIDI YA PRISONS LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top