• HABARI MPYA

  Friday, February 03, 2017

  NI CAMEROON NA MISRI FAINALI AFCON 2017, GHANA YAPIGWA 2-0

  TIMU ya taifa ya Cameroon itakutana na Misri katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ghana usiku wa jana katika Nusu Fainali ya pili Uwanja wa Franceville mjini Franceville, Gabon.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Michael Ngadeu-Ngadjui na Christian Bassogog wakiiwezesha timu ya Hugo Broos kwenda fainali ya kwanza tangu mwaka 2008.
  Simba Wasiofungika walistahili ushindi huo kutokana na kutawala mchezo kuanzia mapema na kuwapoteza kabisa Black Stars.
  Mfungaji wa bao la kwanza la Cameroon, Michael Ngadeu-Ngadjui akipongezwa na Benjamin Moukandjo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Ngadeu-Ngadjui akifungia bao la kwanza Cameroon dakika ya 72 kabla ya Bassogog kufunga la pili dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
  Kikosi cha Cameroon kilikuwa: Ondoa, Fai, Ngadeu-Ngadjui, Teikeu, Oyongo - Siani, Djoum/Mandjeck dk77, Zoua - Moukandjo, Ndip Tambe/Aboubakar dk73 na Bassogog.
  Ghana: Razak, Acheampong, Boye, Amartey, Afful - Wakaso, Acquah/Gyan dk76, Partey/Agyemang-Badu dk86, Atsu, A.Ayew na J.Ayew.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI CAMEROON NA MISRI FAINALI AFCON 2017, GHANA YAPIGWA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top