• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2017

  MCHEZAJI WA ZAMANI YANGA, TAIFA STARS GEOFFREY BONNY AFARIKI DUNIA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Geoffrey Bonny Namwandu (37) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
  Dada wa mchezaji huyo wa zamani wa Prisons ya Mbeya na Yanga SC ya Dar es Salaam, Neema ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wamempoteza kipenzi chao baada ya kuhangaika naye kumuuguza kwa muda mrefu.
  Neema amesema kwamba msiba upo nyumbani kwao mjini Mbeya ambako taratibu za mazishi zimekwishaanza.
  Godfrey Bonny (kulia) akibadilishana jezi na Bruno Batista wa Atletico Paranense ya Brazil baada ya mchezo wa kirafiki Januari 2011 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

  Geoffrey Bonny hali yake ilivyokuwa siku za mwisho za uhai wake 

  Bonny alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars enzi za kocha Mbrazil, Marcio Maximo na wengi wanamkumbuka kwa soka yake maridadi katika sehemu ya kiungo, licha ya kwamba aliibuliwa wakati umri wake umekwishaenda.
  Alicheza Yanga chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Kondic na akaendelea hata alipoondolewa mwalimu huyo na kuletwa Mseribia mwingine, Kostadin Papic.
  Timu ya mwisho ya Geoffrey Bonny kuchezea, Simrik SYC ya Nepal      
  Geoffrey Bonny (wa pili kulia waliosimama)  akiwa kwenye kikosi cha Simrik SYC ya Nepal. Wa pili kushoto waliosimama ni mchezaji mwingine wa Tanzania, Pius Kisambale  
  Geoffrey Bonny akiichezea Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN mwaka 2009

  Ni kati ya wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kukata tiketi ya kucheza fainali pekee za michauno ya Ubingwa wa Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.  
  Hata hivyo, Maximo akamtema katika kikosi cha Stars baada ya fainali za CHAN nchini Ivory Coast mwaka 2009 kutokana na kuwa majeruhi.
  Maumivu hayo yalimfanya aachwe na Yanga mwaka 2011 akaenda kumalizia soka yake Simrik SYC ya Nepal.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA ZAMANI YANGA, TAIFA STARS GEOFFREY BONNY AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top