• HABARI MPYA

    Sunday, February 12, 2017

    MTIBWA SUGAR YABANWA NA LYON, SARE 2-2 SHAMBA LA BIBI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MTIBWA Sugar leo imecheza mechi ya nne bila ushindi, baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji, African Lyon katika amchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja kila timu, Mtibwa Sugar ikifikisha pointi 32 na Lyon pointi 22 baada ya timu zote kucheza mechi 22 hadi sasa.
    Nahodha Hassan Isihaka alianza kuifungia African Lyon dakika ya 33 kwa penalti baada ya mshambuliaji Venence Joseph Ludovic kuangushwa na Henry Joseph Shindika kwenye boksi wakati anaiwahi pasi ya Peter Mwalyanzi.
    Mshambuliaji mwenye mwili mkubwa, Stahmili Mbonde akaifungia Mtibwa Sugar bao la kusawaisha dakika ya 68 baada ya kuwatoka mabeki wanne wa Lyon kufuatia pasi ya beki wa kushoto, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
    Lilikuwa bao zuri ambalo linastahili kufikiriwa kwenye orodha ya mabao bora ya Ligi Kuu msimu huu. 
    Kiungo Ibrahim Rajab ‘Jeba’ akaifungia Mtibwa bao lililoeleeka kuwa la ushindi dakika ya 53 kwa kichwa akimalizia mpira wa adahbu wa Baba Ubaya kutoka upande wa kushoto.
    Henry Jospeh akamuangusha tena Venence Ludovic kwenye boksi dakika ya 71 na refa Mathew Akrama wa Mwanza akawapa penalti nyingine Lyon, ambayo ilikwenda kufungwa tena na Hassan Isihaka dakika ya 72.
    Hali si nzuri kwa Zubery Katwila anayekaimu Ukocha Mkuu wa timu baada ya Salum Mayanga kuchukuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya timu ya taifa, Taifa Stars.
    Kwanii huu ni mchezo wa nne timu inacheza bila kushinda, ikitoa sare mbili na kufungwa mbili, ingawa mechi tatu imecheza ugenini. Ilitoa sare ya 0-0 na Simba Morogoro, ikafungwa 2-1 na Kagera Sugar Bukoba na 5-0 na Mbao FC mjini Mwanza kabla ya sare ya leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YABANWA NA LYON, SARE 2-2 SHAMBA LA BIBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top