• HABARI MPYA

  Thursday, February 09, 2017

  'MSHKAJI' WA SAMATTA AIFUNGIA LEICESTER CITY IKIUA 3-1 KOMBE LA FA ENGLAND

  Mchezaji mpya wa Leicester City, Mnigeria Wilfred Ndidi (katikati) aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka KRC Genk ya Ubelgiji alipokuwa anacheza na Mtanzania, Mbwana Samatta akifumua shuti kuifungia timu yake mpya dakika ya 94 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Derby County baada ya kuingia kutokea benchi Uwanja wa Kings Power na kutinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA England. Mabao mengine ya Leicester yalifungwa na Andy King dakika ya 46 na  Demarai Gray dakika ya 114 katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1. Bao la Derby lilifungwa na Abdoul Camara dakika ya 61 na sasa Leicester itapambana na timu ya Daraja la Kwanza, Millwall katika hatua ijayo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'MSHKAJI' WA SAMATTA AIFUNGIA LEICESTER CITY IKIUA 3-1 KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top