• HABARI MPYA

    Thursday, February 02, 2017

    MESSI, SUAREZ WAINYAMAZISHA ATLETICO MADRID VECENTE CALDERON

    Washambuliaji Luis Suarez (kulia) na Lionel Messi (kushoto) wakipongezana baada ya wote kufunga katika ushindi wa 2-1 wa Barcelona dhidi ya Atletico Madrid usiku wa jana kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania. Suarez alifunga dakika ya saba akimalizia pasi ya Javier Mascherano na Messi dakika ya 33 akimalizia pasi ya Ivan Rakitic, kabla Antoine Griezmann kuifungia Atletico dakika ya 59 akimalizia pasi ya Diego Godin. Barcelona sasa watakuwa wenyeji wa Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano Jumanne Uwanja wa Nou Camp PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI, SUAREZ WAINYAMAZISHA ATLETICO MADRID VECENTE CALDERON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top