• HABARI MPYA

    Thursday, February 16, 2017

    MAVUGO AIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI KOMBE LA ASFC

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la Laudit Mavugo leo limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi, alifunga bao hilo dakika ya 57 baada ya kumzidi maarifa beki wa Lyon, Hassan Isihaka na kufumua shuti dhaifu lililompita kipa Mcameroon, Rostand Youthe kufuatia pasi ya mshambuliaji Ibrahim Hajib.  
    Simba SC sasa inakuwa timu ya kwanza kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo, hatua ambayo walikomea msimu uliopita baada ya kutolewa na Coastal Union ya Tanga. 
    Laudit Mavugo akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Simba bao pekee leo
    Ibrahim Hajib akiwatoka wachezaji wa African Lyon
    Laudit Mavugo akifumua shuti pembeni ya Miraj Adam
    Mohammed Hussein 'Tshabalala' wa Simba akienda chini baada ya kukwatuliwa na Peter Mwalyanzi wa Lyon
    Said Ndemla wa Simba SC akimtoka kiungo wa Lyon

    Hiyo ilifuatia dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Lyon wakicheza kwa kujihami zaidi na kuizuia kabisa Simba kupata bao.
    Lyon hawakuwa na shambulizi la maana katika mchezo huo hadi walipofungwa na walipaozma kujaribu kupeleka mipira langoni mwa Simba.
    Lakini leo safu ya ulinzi ya Simba inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog iliyoongozwa na Novaty Lufunga na Abdi Banda ilikuwa makini.
    Kiungo aliyetokea benchi kipindi cha pili Mohammed ‘Mo’ Ibrahim almanusra aipatie Simba bao la pili dakika ya 84 kama si mpira aliopiga kwa kichwa mpira kugonga mwamba kufuatia krosi ya beki Mkongo, Janvier Besala Bokungu.
    Kikosi cha Simba kilikuwa: Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Jonas Mkude, Novaty Lufunga, James Kotei, Said Ndemla/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk70, Laudit Mavugo/Pastory Athanas dk85, Ibrahim Ajibu na Juma Luizio/Shiza Kichuya dk59. 
    African Lyon: Rostand Youthe, Miraji Adam, Baraka Jaffary, Omary Salum, Hamad Waziri, Hassan Isihaka, Peter Mwalianzi, Hamad Manzi/Awadh juma dk49, Rehani Kibingu, Venance Joseph na Omary Daga/Fred Cossmas dk72.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAVUGO AIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI KOMBE LA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top