• HABARI MPYA

  Wednesday, February 08, 2017

  MATUMLA ATAKIWA KUPUMZIKA MWAKA MZIMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BONDIA Mohammed Matumla ametakiwa kupumzika kwa miezi 10 hadi 12 kufuatia kupigwa Knockout (KO) mbaya na Mfaume Mfaume Februari 5, mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
  Matumla alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya raundi 10 na ya mwisho kupigwa KO mbaya kufuatia kusukumiwa ngumi nyingi mfululizo kichwani na Mfaume Jumapili.
  Mtoto huyo wa bondia gwiji wa zamani nchini, Rashid Matumla alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Muhimbili, kabla ya juzi kutolewa na kuwekwa wadi ya kawaida.
  Mohammed Matumla (kulia) ametakiwa kupumzika kwa miezi 10 hadi 12 kufuatia kupigwa KO na Mfaume Mfaume  

  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, baba na kocha wa bondia huyo, Rashid ‘Snake Man’ Matumla alisema kwamba hali ya mwanawe sasa inaendelea vizuri, lakini Daktari amesema atatakiwa kupumzika kwa miezi 10 hadi 12.
  Akizungumzia kilichotokea kwenye pambano hilo, Matumla alisema kwamba ngumi ni michezo kama mingine, unatakiwa kuwa makini mwanzo hadi mwisho, kitu ambacho anadhani mwanawe alikosa.
  “Moudy (Mohammed) aliongoza pambano vizuri sana na alikuwa anasubiri sekunde chache tu liishe atangazwe mshindi kwa pointi. Lakini akasahau anapigana na bondia mwenye mkono mzito, matokeo yakawa hivyo. Ni mambo ya kawaida katika michezo,”alisema.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MATUMLA ATAKIWA KUPUMZIKA MWAKA MZIMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top