• HABARI MPYA

  Friday, February 10, 2017

  MANJI YUKO RUMANDE TANGU JANA, KAMANDA SIRRO ASEMA...

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji yuko rumande tangu jana kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema leo mchana akizungumza na Waandishi wa Habari kwamba Manji yuko rumande tangu jana akiendelea kuchunguzwa.
  Na hiyo ni baada ya Manji kujisalimisha mwenyewe jana baada ya kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika orodha ya watu 65 wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
  Makonda aliwataka wote 65 kufika kituo cha Polisi kati leo, lakini Manji akaamua kutangulia jana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI YUKO RUMANDE TANGU JANA, KAMANDA SIRRO ASEMA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top