• HABARI MPYA

  Monday, February 13, 2017

  MANJI AWARUDISHA KUNDINI HASHIM, MKEMI NA NYENZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Yanga SC, umewasamehe na kuwarejesha kundini wanachama wake watatu, Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah na Salum Mkemi ambao walisimamishwa katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka jana.  
  Taarifa ya Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji ametoa msamaha kwa wanachama hao, ambao pia walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
  Katika mkutano Mkuu wa dharula wa Yanga SC Agosti 6, mwaka jana, Manji mwenyewe aliwafukuza uanachama Mkemi, Abdallah na Nyenzi kwa sababu alisema hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji.
  Hashim Abdallah (kulia) alisimamishwa uanachaam wa Yanga katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka jana

  Manji aliwaambia wanachama wa Yanga wanaowataka akina Abdallah, Mkemi na Nyenzi wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.
  Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka. Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.
  Kwa sasa, Manji anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini kwa mahojiano kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watu 65 wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AWARUDISHA KUNDINI HASHIM, MKEMI NA NYENZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top